Swahili Tales/Mashairi ya Liongo

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
Swahili Tales  (1870)  by Edward Steere
Mashairi ya Liongo

[ 456 ]

MASHAIRI YA LIONGO.


Nabudi kawafi takhamisi kidiriji,
Niwathihishe izagale kama siraji,
Ili kufuasa ya Liongo simba wa miji.

Ai wanji wanji nazawanji kisiza wanji; ma kadiliza kasiliza, mwanangwa mema.


Pindi uonapo ali shari mume mwendo,
Pindua mtima nutie kani na vindo,
Uwe ja namire, tui mke, katika shindo.

Mwanangwa mbonaye mbuzi wako katika mwendo; uki­metwa pembe na mkami akimkamaa.


Akhi ewe mbuya twambe mambo ya kujelele,
Huyu muungwana shati ’ari haiondole,
Nakuchea kufa mwenyi cheo kavilikele.

Mwanangwa mbonaje muhakara wakwe wiimile; asirathi kufa na mayuta yakaya nyuma.

[ 458 ]

Naapa kwa Anjili na Zaburi ili kiapo,
Simke ngeufu pindi shari liwagazapo,
Naye keeza moyo katokoza shari lilipo.

Mtetea cheo mwenyi cheo ateteapo; hambiwi ni nawi hatta roho nengakoma.


Naitenda mja kwa wenzangu kapata sono,
Wala sina yambo siwatayi kwa mavongono,
Bali sikubali lenyi thila na matukano.

Ni mwofu wa ta nishikapo na oa mno; ni mui wa kondo sikiapo mbi kalima.


Siwagazi kondo msi lango kapiga kifa,
Hi kusifua kwambazo ni tule swifa,
Nitangamizapo kondo nzito tenda hakhafa.

Ni mwana shajighi mpendeza nyemi za kufa; kwa kucha mpeo na adui wa kunisema.


Bonapo harubu kiugua nawa na afya,
Kawana furaha ja arusi ya mzofafa,
Naikeza moyo kwa Muungu nisikhilafa.

Ni mwana asadi mpendeza nyemi za kufa; kwa kucha mpeo na adui kumbuya nyuma.

[ 460 ]

Napa kwa Miiuugu na Muungii ili kiapo,
Nampenda mtu pindi naye auipendapo,
Bali ndngii yangu 'ari punde ambagazapo.
Ninga mana kozi sioneki niwakuapo ; ni mui wa nyuni
naakua katika jama.

Wallalhi nitliiika saya yangu si maongope,
Teteapo cheo kiwa muyi uawa meupe,
Nimpapo iiso aduiye sliatti akope.
Ninga mana taya sliirikeni na mana tope ; na mlislia
yani lenyi tani na zingulima.

Laiti kiunibe pindi mambo yakimpinga,
Papale angaui aduise akawaenga,
Awavunda paa na mifupa ya mitulinga.
Niugali kipungii niusbile katika anga ; kila uyama toto
hatta simba mkuu nyama.

Ningatindangile kwa sayufu na kwa sakini,
Na musu mkali kiiipeka juu na tini,
Kivuma ja niwamba usokaa nili na kani.
Bali muu yangu yu mawili kuwa pinguni ; ua sbingoni
mwaugu nawisbiwa peto la chuma.

[ 462 ]

Ningashahadize Korani yangu kalina,
Ilia uketeze kuwa uyimbo Mola karima,
"Wamá litiwa bi skairi kalilama."
Tufutufu mayi kizimbwiui yawanguruma ; ha'mwezi
kwima luiskapo wdmbi Ungama.

Ata maagano na makato ujikatayo,
Sangase mkono kumtenda akutendayo,
Kumlipa deni mtu kata akujiasayo.
Sipepese moyo kupepesa kwa uuwayo ; mtawapoua aduizo
wakula nyama.

Sange kumtenda mnitenda mawi yetama,
Kama chiambileo chuonimwe mwenyi atliama,
"Wa in 'akabitiim fakakibu bi mitbilima."
Pindi uonapo moto zita ukinguruma ; la Allah, ni mimi
niwashao maa kazima.

Nyani muurudi moyo waugu hukisakawi ?
Teteapo cheo hatta mtu simtambui,
Ninga watu sao ja mfano kama badui.
Naikutakuta kayatia katika wawi ; katinda kitinda ari-
thisha wangu mtima.

[ 464 ]

Ewe mbasi yangu twambe kwamba huitabiri,
Kiuinbe mweuzio huwezaye iaikuhasiri ?
Tetea hakio ujitie katika sbari.
Siche mata yao ua mafumo yanganawiri ; maugi mafumati
na magao maoya nyuma.

Ni upi mchayi kicho cliakwe kimokoao ?
Na mjaliasiri umurie ipuuguwao ?
Mwauzi ata kicho na wacbao saudauye nao,
Wangapi wachao utamboni waugamiao ; na wazimbiao
utamboni wakisiama.

Bolewe mchayi mcha kufa asiofikira,
Na kufa si suna ni faratbi ya mkadara,
Bolewe mchayi mcha kufa bapati 'ura.
Akuta mpeo na bizaya na mubakara ; kwa kuchea roho na
mwisoe yaja kutama.

Nionapo 'ari ulimwengu wanitukiza,
Moyo ukiuayi batta ndani ukawa kiza,
Na nde mwa kope tozi tule likituuza.
Simba uwalia kwa kilio akivumiza ; kilio kikuu
kifishacho mtu huruma.

[ 466 ]

Kilizacho simba ni matule kulla matufu,
Simba uwalia elewani nawaarifu,
Sithanie simba muu mane wenda 'arufu
Simba bora ndume watetea jalia na cheo; watetea jaha
hatta mato yakafunama.

Ana mi shujaa simba uclole mwondoa 'ari,
Mvunda kilaa na busimi kizidabiri,
Naipiga kifa baitia katika sbari.
Sichi mata zao na mafumo yanganawiri ; mangi mafumati
na magao mawi ya nyuma.

Ana ndimi simba mfiliye jaba na cheo,
Naipiga kati kawanesa wajibagao,
Sicbe aduizo kukutana kwa ungi wao.
Sichi kikwi chao nami imie ndio nilio moyo waugu kikwi
kwa ajili ya kusbagama.

Ndimi akabiri uteteo wangu murua,
Thili siikii-i ya kiumbe mnknlukna,
Naakua anjari penyi kikd kaisbambna.
Kifa tenda ngao paziwapo kipazua ; nisikbofu miwa wala
tome za kunitoma.

[ 468 ]

Mwanzi ata kichio na wachao sendanye nao,
Nao fawitlii umuri kwa Muungu anusurao,
Siche ya ziumbe na zituko wakutishao.
Kufa kwa Muungu na sliabuka limkutao ; si kwa wali-
mwengu mivi kikwi ingakufuma,

Watetea jalia woka nyoyo wasio changa
Watwa miwili wakalisha misu na panga
Waondoao thuli penyi 'ari wakaitenga.
Si simba mikia wameao vuzi na singa; siniba masliujaa
wasabili ngozi na nyama.

Tamati nishize takhamisi kinaatbimu
Ya Lionga fumo nimaziye kuikbitimu,
Mwona lahani akitoa baua laumu,
Wapata ajira kumlipa Mola karimu; siku ya majaza wali-
pwapo wawi na wema.

[ 470 ]

Na mwenyi kutunga mbaarifu yakwe isimu,
Ni Abdallah Muyuweni mumfahamu,
Ibun Ali bun Nasiri mwenyi makamu,
Farii ya Makka shimukati lao Farimu; fungu la Muthari,
Mutalibu na Hashima.

Nipulikizani na sabuye niwakbubiri
Ni Ali Sbeklii maulana Abubakari,
Ibun Salim mauusabu ya kukhitari,
Mungi wa karama buruhani na mashuhuri ; kwa zamani
zakwe hakwalina kamaye kama.

[ 456 ]


[ 456 ]

The same in ordinary Swahili.

Nandiliza ushairi wa utanu nikipita kwa upesi,
Nipambanue utoe nuru kama taa,
Kwa ajili kufuata Liongo simba wa miji.

Ee ungi ungi naanza kwa wengi; pamoja na ukiandaliza nikaishiliza kizao cha mambo mema.


Pindi ukiona mwenyi ubaya mume mwenziwo,
Geuza moyo uvike bidii na machungu,
Iwe kama chui, chui mke, katika kundi.

[ 457 ]

Mtoto waonaje mbuzi wako katika mwendo amekamatwa pembe na mkami akimkama.


Ndugu yangu, ewe rafiki, tuseme mambo yamekujalia,
Huyu mungwana shuruti jambo la kufathaika aiondoe,
Nakuogopa kufa mwenyi daraja havikuelekea.

Mtoto wangu waonaje unyonge wake husimama; asirithie kufa na majuto yakaja nyuma.

[ 458 ]

Nappa kwa Anjili na Zaburi ni viapo thabiti,
Simpi mgongo pindi ubaya ukinikabili,
Naye hukabilisha moyo haitafuta ubaya papo pote.

Agombeaye daraja mwenyi daraja zamani agombeapo uovu na uovu hatta roho nengafikilia ajali.


Najifanyiza mtumwa kwa watu kama mimi nipate heshima,
Wala sina jambo nao siwataji kwa kuamba,
Lakini sikubali lenyi unyonge na matukano.

Huyeyuka kama nta nishikwapo huyeyuka mno, ni muovu wa vita pindi nikisikia mabaya maneno.

[ 459 ]

Siingii katika vita nisipokuwa na jambo kupiga kifua,
Kwa ajili ya kusifiwa ambazo ni mbaya sifa
Hitegemea vita bora huvitenda khafifu.
Mimi ni mwana shujaa nipendaye mapenzi ya kufa, kwa
kuogopa hizaya na adui wa kunisema.

Nikiona vita nikiugua naona afya,
Nikaona furaha kania harusi siku ya kutiwa nyumbani,
Huwelekeza moyo kwa Muungu jjasipo kinyuma.
Mimi ni mwana wa simba, apendaye mapenzi ya kufa, kwa
kuogopa hezaya na adui kuniona nyuma ya watu.

[ 460 ]

Naapa kwa Muungu na Muungu ni kiapo,
Nampenda mtu maadam naye anipendapo,
Lakiui ndugu yangu ari kidogo anikuvizapo.
Ni mfano wa mtoto wa kipauga sionekani nikamatiipo ; ni
mbaya wa ndege uakamata katika jamaa.

Mimi nikaapa nikifungwa bora yangu si uwongo,
Nigombeapo daraja akiwa mbaya mwenzi buwa mweupe,
Nikimkabili kwa uso adui sburuti aiinyane.
Huwa kama mtoto wa nyama ya mwitu aliyesbarikana na
mana wa mwitu ua mlisba majaui ya maboonde na ya
vilima.

[ 461 ]

Kutamani kiumbe pindi mambo yakimpinga,
Pale jangwani adui zake akiwaona,
Awavuuja utosi na mifupa ya mitulinga.
Ningalikuwa ndege mkali nikiruka maingaingani, nikila
nyama vidogo hatta simba mkuu wa nyama.

Ningaliwakatakata kwa panga na kwa kisu,
Na sime mkali nikiipeleka juu na chini,
Nikivuma kama mwamba usio pahali pa kuingilia
ghathabu na machungu.
Lakini miguu yangu yote miwili kuwa pinguui ; na
shingoni mwaugu nimevikwa mnyoo wa chuma.

[ 462 ]

Ningalishudiza Korani yangu maneno
Lakini amekataza kuwa nyimbo Mola Karimu,
Hakuwaye kuwa mwimba nyimbo kabisa.
Cheumkoclieumko la maji katika kilindi zangurnma ;
ha'mwezi kusimama lirushapo wimbi katika
Ungama.

Acha mashuari na matendo ya moyo ujitendao,
Usizuie mkono kumtenda mambo akutendayo,
Kumlipa deni mtu kipimo akukopesheayo;
Usitie wasiwasi moyo kutagliafali na uuwaye ; na kwamba
hukuua aduizo watakula nyama.

[ 463 ]

Siogopi kumtenda anitendaye mabaya ya uovu,
Kama alivyotuhubiri katika chao chakwe mwenyi ukuu,
"Ya unitendapo tendani kana mlivyotendwa"
Pindi uonapo moto wa vita ukinguruma, la Allah nikawa
mimi niuwashao pamoja nikauzima.

Nani aurudiye moyo wangu uwishapo twaa nguvu?
Nigombeapo cheo hatta mtu simtambui,
Ni kama watu hao mfano wao kama mabedawi.
Najikuujakunja nikajitia katika wabaya; nikachinja ki-
chinja nikaupa rathi moyo wangu.

[ 464 ]

Ewe rafiki yangu tuseme kwamba zingatii,
Kiumbe mwenzio buwezaje kukuhasiri?
Gombea baki yako ujitie katika sbari.
Usiogope mishale yao na mikuki na ingang'ara; wangi
hupiga chini na geukao na warudiao nyuma.

Nani aogopaye kicbo chake kikamponya?
Na mtu mjasiri umri wake upungukao?
Ee raliki acba kbofu na waogopao usifuataue nao.
Wangapi waogopao vitani wakafa, na wasimamao vitani
wakavuka.

[ 465 ]

Ole wake mwoga aogopaye kufa asiyekuwaza,
Na kufa si sunna ni farathi ya iliokadiriwa,
Ole wake mwoga aogopaye kufa hapati heshima,
Akuta mpeo na hizaya na unyonge kwa kuogopea roho, na
mwisho wake waja kuhama.

Nikiona ari, ulimwengu wauichukiza
Moyo ukinayi hatta ndani ukawa na kiza
Na nje ya kope chozi la unyonge likipita.
Simba hulia kwa kilio, akivumiza kilio kikuu kimtiacho
mtu huruma.

[ 466 ]

Kilizacbo simba ni manyonge killa maovu,
Simba hulia fabamuni nawaambia,
Si nitbanie simba mwenyi miguu minue afuataye arufu.
Simba bora ndume bugomboa jaba na cheo, hugombea jaba
batta macho yakafumbaua.

Mimi shujaa simba mwenyi kucba aondoaye ari,
Avundaye gereza na ugome kwa biLa,
Hujipiga kifua chaugu nikajitia katika shari.
Siogopi nyuta zao ua mafumo na ingameta ; wengi
waliotandika chini na wenyi kukimbia wanaorudi kwa
nyuma.

[ 467 ]

Mimi ndimi simba nifaaye jaha na daraja,
Najitia kati nikawathilislia wanaojisifu;
Usiogope adui zako wakikutana kwa wingi wao.
Siogopi alafa zao nami peke yangu ndio nilio moyo waugu
alfu kwa ajili ya kuwa thabiti.

Ndimi mkubwa mgombea yangu heshima,
Unyonge sikubali ya kiumbe aliyeumbwa,
Natoa jambia penyi elfu nikajitupa kwao.
Kifua nitatenda ngao wazibwapo nikawazibua, nisiogope
miiba wala kombo ya kunichoma.

[ 468 ]

Rafiki acha uoga na waogopao usifuatane nao,
Nao mwachie maisba kwa Muungu aponyaye,
Usiche mambo ya viumbe na kbofu yakuogofishayo.
Kufa ni kwa Muungu na sbabuka yarapatao; si kwa
walimwengu, mishare alfu ikikuchoma.

Wagombea jaba zimenyoka nyoyo wasioogopa malaana,
Hutwaa maungo wakalisba sime na panga,
Waondoao unyonge penyi ari wakaiwcka kando.
Si simba mwenyi mkia waotao nyele za sbingo na mgongo,
lakini simba ni watu masbujaa waacbiliao ngozi na
nyama.

[ 469 ]

Imekoma, nimeisha shairi la vituo vitano ninaotunga,
Za Liongo jumbe nimekwisha kuimaliza.
Aonaye neno la kuharibika akiliondoa hana matayo,
Hupata ajira atakayomliim Muungu mpaji siku ya kuja-
ziwa walipwapo wabaya na wema.

[ 470 ]

Na mwenyi kutunga nawaarifu jina lake,
Ni Abdallah Muyuweni iwelee,
Ibun Ali bun Nasiri mwenyi utukufu,
Utawi wa Maka, asili ya chimbuko lao Farimu, kizao
cha Mutbari, Mutalibu na Mashima.

[ 471 ]

Nisikilizeni kabilaye niwahubiri,
Ni Ali Shekhi seyidi yetu Abubakari
Ibun Salim daraja ya kukhitari,
Mwingi mwenyi kabuli dalili zake zi wazi, kwa zamani
zake hakupatikana mfano wake mfano.