Page:Swahili tales.djvu/487

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
POEM OF LIONGO





Mimi ndimi simba nifaaye jaha na daraja,
Najitia kati nikawathilislia wanaojisifu;
Usiogope adui zako wakikutana kwa wingi wao.
Siogopi alafa zao nami peke yangu ndio nilio moyo waugu
alfu kwa ajili ya kuwa thabiti.

Ndimi mkubwa mgombea yangu heshima,
Unyonge sikubali ya kiumbe aliyeumbwa,
Natoa jambia penyi elfu nikajitupa kwao.
Kifua nitatenda ngao wazibwapo nikawazibua, nisiogope
miiba wala kombo ya kunichoma.