Swahili Tales/Kisa cha Kihindi

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
Swahili Tales  (1870)  by Edward Steere
Kisa cha Kihindi
English translation: An Indian Tale
[ 140 ]

KISA CHA KIHINDI.


Aliondokea Sultani wa Kihindi, akazaa mtoto mmoja, akimpenda sana. Hatta alipokufa, akaagiza mawaziri yake, ufalume mpeni mwanangu, naye mmpende sana, kana mimi. Akafa.

Wakaondoka matanga, akatawala mtoto. Na waziri ana mtoto wake, wakipendana sana wale vijana, wakatumia mali siku nyingi, wakatumia na ufalme.

Hatta siku moja, mtoto wa Sultani akamwambia mtoto wa waziri, na tusafiri, tukaangalie miji. Akamwambia, haya. Wakafanya marikabu, ikapakia vyakula, na fetha, na askari, wakasafiri.

Hatta baharini wakavunja, wakafa watu katháwakatha. Mtoto wa waziri akaliwa na papa, na yule mtumwa wake mmoja akachukuliwa kwa maji. Akapona yeye mtoto wa Sultani, na mtumwa wake mmoja. Wakaangukia mji mgeni.

Walipofika mjini wakakaa mashamba. Yule mtoto wa Sultani akamwambia mtumwa wake; enenda mjini, katafute vyakula, tuje tule.

Alipofika mjini kuna machezo, wamekusanyika watu wangi. Sultani wa mji ule amekufa, wanatafuta Sultani mgine ku'mweka. Hutupa ndimu itakayempiga marra tatu ndiye Sultani.

[ 142 ]Ikatupwa marra ya kwanza. Ikampiga yule mtwana. Wakamtazama, wakanena, haifai, tupeni marra ya pili. Wakatupa. Ikampiga yeye yule mtwana. Wakamwondosha pale alipokuwa, waka'mweka mahali mbali. Wakatupa tena marra ya tatu. Ikampiga yeye yule. Wakanena, bassi, huyu ndiye Sultani wetu.

Wakamchukua wale mawaziri yule mtwana. Wakaenda naye mjini, kwa furaha, na machezo, na mizinga mingi ikapigwa. Wakamtawaza ufalme, akakaa kitako raha.

Mle mjini mna bedui, huchinja nyama akiuza ya mbuzi. Na watu huchinja, akitanganya pamoja, ndio kazi yake, na wale waliomo mjini hawana khabari ile.

Yule mtoto wa Sultani akaja mjini, akapita mlangoni kwa bedui. Akamkamata akamtia ndani, akamfunga mkataleni. Akaona watu wengi wamefungwa na mbuzi. Hatta assubui akatwaliwa mtu mmoja na mbuzi, wakachinjwa. Akatanganya nyama, akaenda akauza barazani. Kulla siku ndiyo kazi yake.

Yule mtoto wa Sultani amekonda kwa hamu, akamwita mtumwa wa yule bedui, akampa sarafu. Akampa, akamwambia, kaninunulie uzi na kitambaa. Akamnunulia, akamletea. Akashona kofia mzuri, akaandika mashairi ndani ya kofia. Akaandika,

Ajabtu rangadida na kitun hiraja Illahi
Eke kordenai, eke kordeshire,
Raja bondekana, gulam batashahi;
Ajabtu rangadida, kitun hiraja Illahi.

Akampa yule bedui. Akafurahi sana. Akamwambia, [ 144 ]enenda kauze kofia hii kwa Sultani, ndipo utakapopata thamani. Akaenda akauza.

Alipoiona yule Sultani, akajua kazi ile ya kofia ni ya bwana wake. Akasoma na yale mashairi, akayajua maana yake, na maana yake hii:

Ajabu ya Muungu,
Mmoja ametwaliwa na maji,
Mmoja ametwaliwa na papa,
Mngwana nimefungwa,
Mtumwa wangu amepata usultani,
Ajabu ya Muungu.

Akamwuliza yule bedui, umeipata wapi kofia hii? Akamwambia, mke wangu ndiye aliyeifanya. Akampa reale khamsini, akamwambia, mwambie mkewo anifanyie nyingine. Akaenda zake yule bedui.

Akatoa askari, akawaambia, mfuateni nyuma, mkimwona nyumba atakayoingia, mrudi, mje mniambie. Wakamfuata hatta kwake. Akaingia ndani. Wale asikari wakarudi. Wakaenda wakamjibu Sultani. Wakamwambia, tumeiona nyumba yake.

Wakatolewa askari mia, wakaenda kwake. Akawaambia, mkamateni mmfunge na watu wote waliopo kwake 'mwalete, kama mje nao. Wakaenda, wakamkamata, wakamfunga, wakaja naye, na watu wote waliomo nyumbani. Akaulizwa, wee ndiyo kazi yako, kukamata watu ukiwafunga nyumbani mwako, kupata kuwachinja, ukiwalisha watu? Asiweze kukana. Wakaulizwa wale, wakanena ndiyo kazi yake. Akafungwa gerezani.

Akamtwaa yule bwana wake, akawaamrisha watu wakamwoga, akampa nguo, akavaa. Akampa chakula, akala, [ 146 ]
akashiba. Akamwuliza habari yake. Akamwambia yote. Na mimi ni Sultani kwa hapa mjini, lakini kesho ntajiuzulu nikupe wewe, bwana wangu, sithubutu kuwa Sultani mbele yako. Akamwambia, vema.

Hatta assubui akakusanya watu wote mjini, wakaenda kwa Sultani. Na yule bwana wake akampamba sana, aka'mvika nguo zile za mfalme. Alipotoka wataajabu watu,—ginsi gani habari hii? Akawaambia, nimewaita kuwaambia, Usultani huu mmenipa kwa kweli ao kwa ubishi? Wakamwambia wale mawaziri, tumekupa kwa kweli. Akawauliza, nilipendalo mimi, na nyinyi mwalipenda? Wakamjibu, twalipenda.

Akawaambia, mimi napenda Sultani awe huyu bwana wangu. Wakamjibu, tumekubali. Wakamwuliza, huyu nani? Akawaambia, huyu bwana wangu halisi, ni Sultani huko kwao, wallakini hii amri ya Muungu.

Wakafurahi sana wale waliomo mjini, na yule bedui akaenda akatoswa, na mali yake yote wakapewa maskini. Wakakaa raha mustarehe hatta khatima.