Page:Swahili tales.djvu/162

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
142
KISA CHA KIHINDI.

Ikatupwa marra ya kwanza. Ikampiga yule mtwana. Wakamtazama, wakanena, haifai, tupeni marra ya pili. Wakatupa. Ikampiga yeye yule mtwana. Wakamwondosha pale alipokuwa, waka'mweka mahali mbali. Wakatupa tena marra ya tatu. Ikampiga yeye yule. Wakanena, bassi, huyu ndiye Sultani wetu.

Wakamchukua wale mawaziri yule mtwana. Wakaenda naye mjini, kwa furaha, na machezo, na mizinga mingi ikapigwa. Wakamtawaza ufalme, akakaa kitako raha.

Mle mjini mna bedui, huchinja nyama akiuza ya mbuzi. Na watu huchinja, akitanganya pamoja, ndio kazi yake, na wale waliomo mjini hawana khabari ile.

Yule mtoto wa Sultani akaja mjini, akapita mlangoni kwa bedui. Akamkamata akamtia ndani, akamfunga mkataleni. Akaona watu wengi wamefungwa na mbuzi. Hatta assubui akatwaliwa mtu mmoja na mbuzi, wakachinjwa. Akatanganya nyama, akaenda akauza barazani. Kulla siku ndiyo kazi yake.

Yule mtoto wa Sultani amekonda kwa hamu, akamwita mtumwa wa yule bedui, akampa sarafu. Akampa, akamwambia, kaninunulie uzi na kitambaa. Akamnunulia, akamletea. Akashona kofia mzuri, akaandika mashairi ndani ya kofia. Akaandika,

Ajabtu rangadida na kitun hiraja Illahi
Eke kordenai, eke kordeshire,
Raja bondekana, gulam batashahi;
Ajabtu rangadida, kitun hiraja Illahi.

Akampa yule bedui. Akafurahi sana. Akamwambia,