Page:Swahili tales.djvu/166

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
146
KISA CHA KIHINDI.


akashiba. Akamwuliza habari yake. Akamwambia yote. Na mimi ni Sultani kwa hapa mjini, lakini kesho ntajiuzulu nikupe wewe, bwana wangu, sithubutu kuwa Sultani mbele yako. Akamwambia, vema.

Hatta assubui akakusanya watu wote mjini, wakaenda kwa Sultani. Na yule bwana wake akampamba sana, aka'mvika nguo zile za mfalme. Alipotoka wataajabu watu,—ginsi gani habari hii? Akawaambia, nimewaita kuwaambia, Usultani huu mmenipa kwa kweli ao kwa ubishi? Wakamwambia wale mawaziri, tumekupa kwa kweli. Akawauliza, nilipendalo mimi, na nyinyi mwalipenda? Wakamjibu, twalipenda.

Akawaambia, mimi napenda Sultani awe huyu bwana wangu. Wakamjibu, tumekubali. Wakamwuliza, huyu nani? Akawaambia, huyu bwana wangu halisi, ni Sultani huko kwao, wallakini hii amri ya Muungu.

Wakafurahi sana wale waliomo mjini, na yule bedui akaenda akatoswa, na mali yake yote wakapewa maskini. Wakakaa raha mustarehe hatta khatima.