Swahili Tales/Mifano

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
Swahili Tales  (1870)  by Edward Steere
Mifano
English translation: Proverbs
[ 192 ]

MIFANO.


Haraka, haraka, haina baraka.

Ulimi hauna mfupa.

Mvundá nti mwaná nti, mgeni mzo mpima.

Kipya kinyemi, kigawa kionda.

Mbio za sakafuni hwishia ukingoni.

Kazi mbi si mtezo mwema?

Si taajabuni, waana Adamu, mambo yalio duniani.

Kilimia kikizama kwa jua, huzuka kwa mvua; kikizama kwa mvua, buzuka kwa jua.

Sahani iliofunikwa, kilichomo kimestirika.

Hakuna msiba asiokuwa mwenziwe.

Angurumapo simba, mteza nani? [ 194 ]Saburi ni ufunguo wa faraja.

Abadi, abadi, ukambaa watinda jiwe.

Ndovu wawili wakisongana ziumiazo nyika.

Udongo upate uli maji.

Mlevi wa mvinyo hulevuka, mlevi wa mali halevuki.

Kikulacho kinguoni mwako.

Maombolezo katika kilio si mwema.

Usubi aweza kupenya mote.

Ametumbukia kisimani.