Page:Swahili tales.djvu/212

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.

MIFANO.


Haraka, haraka, haina baraka.

Ulimi hauna mfupa.

Mvundá nti mwaná nti, mgeni mzo mpima.

Kipya kinyemi, kigawa kionda.

Mbio za sakafuni hwishia ukingoni.

Kazi mbi si mtezo mwema?

Si taajabuni, waana Adamu, mambo yalio duniani.

Kilimia kikizama kwa jua, huzuka kwa mvua; kikizama kwa mvua, buzuka kwa jua.

Sahani iliofunikwa, kilichomo kimestirika.

Hakuna msiba asiokuwa mwenziwe.

Angurumapo simba, mteza nani?