Page:Swahili tales.djvu/214

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
194
MIFANO.

Saburi ni ufunguo wa faraja.

Abadi, abadi, ukambaa watinda jiwe.

Ndovu wawili wakisongana ziumiazo nyika.

Udongo upate uli maji.

Mlevi wa mvinyo hulevuka, mlevi wa mali halevuki.

Kikulacho kinguoni mwako.

Maombolezo katika kilio si mwema.

Usubi aweza kupenya mote.

Ametumbukia kisimani.