Swahili Tales/Vitendawili

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
Swahili Tales  (1870)  by Edward Steere

English translation: Enigmas

Kamba yangu ndefu haifungi kum

[ 418 ]

VITENDAWILI.


Kitendawili!————Tega.

1. Nyumba yangu kubwa, haina mlango.
Yayi.

2. Kuku wangu akazalia miibani.
Nanasi.

3. Tandika kitanga, tule kunazi.
Nyota.

4. Anatoka kutembea, anakuja nyumbani, anamwambia, mama nieleke.
Kitanda.

5. Kombe ya sultani i wazi.
Kisima.

6. Watoto wangu wana vilemba, asio kilemba si mwanangu.
Fuu.

7. Kafunua jicho kundu.
Jua.

[ 420 ]8. Nikitoka kutembea, nikashika ng'ombe mkia.
Kata.

9. Nyama ya reale haijai kikombe.
Mkufu.

10. Hausimiki, hausimami.
Mkufu.

11. Nimepanda koonde yangu kubwa, nimevuna, hauja mkono.
Nyele.

12. Parra hatta Maka.
Utelezi.

13. Popo mbili zavuka mto.
Macho.