Page:Swahili tales.djvu/438

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.

VITENDAWILI.


Kitendawili!————Tega.

1. Nyumba yangu kubwa, haina mlango.
Yayi.

2. Kuku wangu akazalia miibani.
Nanasi.

3. Tandika kitanga, tule kunazi.
Nyota.

4. Anatoka kutembea, anakuja nyumbani, anamwambia, mama nieleke.
Kitanda.

5. Kombe ya sultani i wazi.
Kisima.

6. Watoto wangu wana vilemba, asio kilemba si mwanangu.
Fuu.

7. Kafunua jicho kundu.
Jua.