Swahili Tales/Simba na kulungu

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
Swahili Tales  (1870)  by Edward Steere
Simba na kulungu
English translation: The Lioness and the Antelope
[ 436 ]

SIMBA NA KULUNGU.


Hapo kale palikuwa na simba, akachukua mimba, akavyaa mtoto. Alipokwisha vyaa mtoto, akashikwa ni njaa siku saba. Akasema, nitatoka kwa nje nitafute chakula. Alipotoka nje akamwona kulungu alisha. Akamnyatia. Yule kulungu akazungusha shingo, akamwona simba, akamwambia, Hachi, mjomba! Huyu simba akafanya haya, saipate kunikamata; amemgeua kumfanyiza mjumbawe.