Swala ya Idd mbili

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search

Tamasha za idd[edit]

Idi za Waislamu ni mbili: Idi ya Fitri baada ya mwezi wa Ramadhani na Idi ya Adh›ha baada ya siku ya Arafa. Na Mwenyezi Mungu Ametupa Idi hizo ziwe ni badala ya Idi za kijahilia na kila idi yenye kuzuliwa. Anas bin Malik t amepokewa akisema: «Watu wa Jahilia (kabla ya Uislamu) walikuwa na siku mbili kila mwaka, wakisherehekea idi hizo. Mtume ﷺ alipokuja Madina alisema: (Mlikuwa na siku mbili mkizisherehekea, na Mwenyezi Mungu Amewabadilishia idi bora kuliko hizo: Idi ya Fitri na Idi ya Adh’ha) [Imepokewa na Nisaa.].

Na haifai kusherehekea wala kushiriki kwenye idi za makafiri. Kwani hizo idi ni alama zenye nguvu zaidi za kila dini na alama zilizojitokeza zaidi za sheria na njia zake. Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Anasema: {Na usifuate mapenzi yao ukaacha haki iliyokujia. Kwani kila mmoja miongoni mwenu tumemuwekea sheria na njia} [5: 48]

Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Ameweka Swala katika Idi mbili hizi inayoitwa Swala ya Idi, nayo ni tukio miongoni mwa matukio yake muhimu zaidi.

Hukumu ya Swalah ya Idi mbili Ni faradhi ya kutosheleza ambayo wakisimama kuifanya watu wanaotosheleza, wengine wasaliao hupomokewa na dhambi ya kutoifanya- na ingawa amri ya kuifanya imetiliwa mkazo sana- Kwani Mtume ﷺ ameamrisha kuitekeleza. Bali aliamrisha kuwatoa wasichana na kina mama, hata wale walioko hedhini (aada ya mwezi) miongoni mwao ingawa hawatoswali. Hii inaonesha ubora wa Swala ya Idi na kuitilia mkazo. Na dalili ya ulazima wake ni yafuatayo:

1. Neno lake Mwenyezi Mungu Aliyetukuka: {Mswalie Mola wako na uchinje} [108: 2].

2. Mtume ﷺ Ameamrisha iswaliwe, mpaka amewaamrisha wanawake waiswali, kwa hadithi iliyopokewa na Ummu ‘Atwiyyah t kuwa alisema: (Ametuamrisha Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ tuwatoe wanawake kwa Swala ya Idi: wadogo wanaoanza kubaleghe [’Awaatiq: ni wingi wa ‘aatiq naye ni msichana mwanzo wa kubaleghe.], waliomo hedhini [ Huyyadh (walio na hedhi): ni wingi wa haaidh (aliye na hedhi).] na wanawali walio paziani [ Dhawaat al- khduur: wanawali (Msichana bikira).]. Ama wenye hedhi watajiepusha na kuswali na watahudhuria kwenye kheri na dua ya Waislamu) [ Imepokewa na Bukhari.].

Viungo vya nje[edit]