Swahili Tales/Mwanzo wa utenzi wa Ayubu

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
Swahili Tales  (1870)  by Edward Steere
Mwanzo wa utenzi wa Ayubu
[ 486 ]

MWANZO WA UTENZI WA AYUBU.


Akhi paui karatasi
Na wino mema mweusi
Na kalamu ya unyasi
Ambayo yaihtariwa.
Na andike nikikutubu
Hadithi ya Kiarabu
Kwa khabari za Ayubu
Tumwa wa Mola Jalia.
Napenda kuwakhubiri
Kiarabu kifasiri
Kwa lugha yetu thabiri
Pasio isiomwelea.
Na maanaye jiiani
Kuyafasiri wendani
Kuna wengi insani
Kiarabu wasiojua.
Ndipo ikanipendeza
Lugha yetu kucheza
Kinuthurau kikutubu
Yalio katika kitabu,
Kwa Kiswahili choua.