Hatta siku ile akaondoka, akaenda kwake, kadiri ya kukaa kitako, paa akatokea. Akiondoka kitandani mbio yule maskini, akaenda akamkumbatia na kulia. Paa akamwambia, nyamaa bwana, silie, nikupe habari nilizo nazo. Ah! paa wangu siku nyingi umepotea, mimi huku nyuma nikalia, nikasikitika, nathania umekufa. Akamwambia, Ah! bwana, mzima mimi, bassi kaa kitako, bwana, nikueleze nalio nayo.
Bwana wake akakaa kitako, akamwambia, haya nieleze. Akamwambia, Bwana ntakueleza mambo, nawe sharti uyaweze. Akamwambia, jambo lo lote utakaloniambia, kwa sababu roho yangu inavyokupenda, ntayaweza utakaponiambia, bwana lale chani, nikupindulie jabali, nami nitalala. Akamwambia, bwana nimeona vyakula vingi, vyakula vya kushiba, vingine vya kuviacha baki, lakini vyakula hivyo vyakula vitamu sana, bwana.
Akamwambia, katika ulimwengu kuna mema matupu? Shuti mema na maovu, ndio ulimwengu, na vyakula ni tamu na uchungu, ndio vyakula vema, viwapo vyakula vitamu tupu, hivyo haviwi vyakula vya sumu?
Akamwambia, bassi sasa tukalale, hatta ussubui nitakapokwenda unifuate. Wakalala, hatta ussubui walipopambauka wakitoka yeye na paa wake, wakaingia katika mwitu. Wakaenda siku ya kwanza, wakaenda siku ya pili, katika mwitu, hatta yalipokuwa siku ya tano katika mwitu, paa akamwambia bwana wake, kaa kitako, napo karibu na mto. Akamtwaa bwana wake, akampiga sana, hatta bwana wake akapiga kelele, Nimetubu, bwana wangu.
Akimwacha pale, akamwambia, usiondoke hapa, mimi