Page:Swahili tales.djvu/90

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
70
SULTANI DARAI.

takia. Marra pale yamekuja yakatandikwa pale. Akamwambia paa, kaa kitako pale. Ah! bwana, hapa patosha nalipokaa, mimi mtumwa wako, mimi kulala chini ni kuona vema, sembuse hapa pametandikwa jamvi. Akamwambia, huna buddi ukaondoke ukakae palepale. Akaondoka akaenda akakaa. Akaamru Sultani kuletewa paa maziwa, akaamru kuleta wali, yakaja maziwa na wali, akala, akaisha wali akanywa na yale maziwa; akaachwa pumzika muda kidogo.

Akamwuliza, nipe khabari yako waliojia. Akamwambia, bwana, nikupe habari naliojia mimi, nimetumwa kuja kukutukana, nimetumwa kuja kukutaka shari, mimi nimekuja kutaka kwako ugomvi, mimi nimetumwa kuja kutaka kwako udugu na ahali.

Sultani akamwambia, Auu! paa, wewe wajua kunena, akamwambia, mimi namtafuta mtu wa kunitukana, mimi namtafuta mtu wa kunisengenya, mimi namtafuta mtu wa kutakana udugu na ahali, nami nimempata kheri, akamwambia, bassi ukanambia maneno yako.

Akamwambia, u rathi Sultani? Akamwambia, elfu marra. Akamwambia, bassi kama u rathi, funua hiyo amana yako. Sultani akainama akaitwaa, akaiweka panapo paja lake, akifungua mwenyewe bi nafsi yake, alipoona almas ile, akataajabu sana Sultani, kwa ginsi yalivyo njema, kwa ginsi inavyotoa nuru. Akaona roho yake Sultani, ametenda zema sana, zisizokuwa na kifani zema zile. Akamwambia, nimeona amana yangu.

Akamwambia, bassi nimekuja na amana hiyo, nimepewa na bwana wangu, Sultani Darai, bassi amesikia, una mtoto