Page:Swahili tales.djvu/84

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
64
SULTANI DARAI.

Ah! vema baba yangu, Muungu akupe huruma. Wakaingia kitandani wakalala yee na bwana wake. Paa siku ile tumbo limeshiba sana majani.

Hatta ussubui walipokucha, akamwambia bwana, naenda zangu, kulisha. Akamwambia, enenda kwa afya na nguvu. Bassi paa akaenda zake, na bwana wake akitoka kwenda zake jaani, wale jirani zake wakimnena. Ah! maskini mwenyi wazimu, labuda huyu mchawi, paa jana siye tukanena hatarudi tena? Kumbe jana jioni akarudi, akalala humuhumu ndani mwake? Sasa hivi ussubui huu, paa ametoka huyu mbio akaenda zake njiani, bassi yale makelele aliyopiga jana, ana wazimo ya kumlilia paa wake, mbona leo amwachia tena? Huyo si burre, nathani ana wazimo, tena wa siri haujawa wa thahiri. Bassi wakaondoka wale jirani, maskini akarudi kwake.

Na yule paa jua lalipokuchwa akarudi nyumbani kwao, amekuta bwana wake amelala anatafuna tumbako, alipokuja yule paa akitwaa mguu wake akawinua aka'mweka nao ndevuni. Akamwita.

Ah! huko utokako kwema? Akamwambia, ah! kwema sana, leo bwana nimekwenda pahali pana majani mazuri, tena pana na mvili, tena pana na baridi, bassi nalipokula majani yale hatta nikashiba, tena pana na faragha, tena pana na mto, bassi hula nikilala nikapunga na upepo, nikatelemka mtoni hinywa maji, hurudi nikaja nikalala, nikapunga na upepo, kazi yalikuwa hii hatta wakati wa kurudi, yalikuwa kazi ya kula, na kulala, na kupunga upepo, kushuka mtoni kunywa maji, hirudi hipunga upepo, bassi roho yangu yanena vema leo, sababu nimestarehe