Page:Swahili tales.djvu/80

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
60
SULTANI DARAI.

yote, kuyafanya ya kunena mimi na mgine kuliko mimi. Wewe sasa huna haja, sikiliza haya ninaokwitia.

Akamwambia, vema, sasa nitasikia, nami nieleze kiada, hatta mambo nisikie.

Akamwambia, la kwanza, mimi nimekukubali kuwa wewe bwana wangu, tena umenigharimia kwa kitu ulichonacho, nami nimeona hali yako thaifu, siwezi kukukimbia wallakini mimi nitakupa wahadi nitakaokwambia, nawe shika.

Akamwambia, Inshallah, wahadi wako utakaonipa utapokuwa mwovu, kwangu mwema, na uwapo mwema, na kwangu zayidi kuliko mwema.

Akamwambia, la kwanza, bwana, nitakwambia wewe bwana maskini, na makuli yako nami bwana nayajua, wewe mwenyewe wayaweza, na kuyaweza kwako ni ukwasefu, bassi kama mimi mtumwa wako wa zakula zile ulazo mimi kwangu ni kuthii wala sina tabassám.

Akamwambia, Bassi wewe wapendaje?

Akamwambia, Bwana wangu, ni mimi nipendalo, nataka uniwie rathi sana, kwani nitanena maneno yatakaokuwa hayakupendezi, ni maneno ya kukasiri.

Amwambia, wewe hukuwa paa tena, umekuwa mwanangu, na uchungu wa mwana ni katika nyongani mwa nina. Akamwambia, bassi wewe unene lo lote ndilo.

Akamwambia, nataka unipe ruksa, mimi tena unisamehe, nataka unipe ruksa nikienda nikilisha hatta jioni, nikirudi nikija nikilala, kama roho yako haistaamani kwa haya nnayokwambia. Kwani yale makuli yako ni machache nami ni kidogo, naye ndio maana nisiweze kukufuata tukila wote, bassi nataka unisamehe tena, na roho yako nayo