Page:Swahili tales.djvu/78

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
58
SULTANI DARAI.

na yule mwaliomnena maskini naye fukara, hohe hahe, hana mbele hana nyuma, naye ameweza yeye kunipunguza mzigo wangu, nanyi wangwana bora hamkuweza akali ya nussu themuni.

Yule maskini akapokea paa wake, akaenda zake pale katika jaa, yeye na paa wake mkononi, akainama kupekua pale jaani, akapata punje za mtama za kutia kinwani mwake, akapata na kidogo punje za mtama akampa paa yake. Akashika njia akaenda zake, akaenda kule nyumbani pale panapo kile kitanda anacholala, akatandika mkeka wake, akalala, yeye na paa wake, pahali pamoja. Hatta usiku ukacha, akaondoka akamchukua na paa wake, akaenda zake hatta palepale jaani, akipekua akapata punje za mtama zinazopata ukufi, akatia kinwani mwake, zaliobaki akampa paa wake. Akaondoka akaenda zake hatta nyumbani kwake, ikapata muda wa siku tano.

Yule paa usiku akinena, akamwita, Bwana! Yule bwana wake akaitika, Labeka, akamwambia, mbona mimi nimeona ajabu?

Paa akauliza, ya nini hii ajabu walioiona hatta ukasituka, hatta ukaghumiwa, hatta ukadaghadagha nafsi yako?

Akamwambia, haya nalioona si haba, ya wewe, paa, kunena.

Akamwambia, wewe umekuupuka na rehema ya Muungu?

Akamwambia, mimi toka asili za baba zetu na bibi zetu na jamii ya watu waliomo katika ulimwengu, sikupata kusikia mtu mmoja kunihadithia kama paa walifahamu kunena.

Bassi, wewe usitaajabu, Mwenyi ezi Muungu anaweza