Page:Swahili tales.djvu/74

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
54
SULTANI DARAI.

Akaondoka yule wa tatu, akanena, Hoo! dalili ya mvua si mawingu? Bassi sisi hatta dalili zake hatukuzipata za kupata huyu.

Akaondoka yule muhadimu, akanena, mimi, waungwana, nitakwenda, kumsikiliza anaoniita, kwani mimi nimetoka tokea kwangu shamba, hatta kufika hapa ndipo, nimekwitwa na watu wengi, hawapungua khamsini ao kama si zayidi, naye hapana mtu mmoja alionunua. Na hawa wote wana mali, si kwamba nga maskini, nao hakununua, bassi nami pia hao nalionyesha wakatazama, wakaisha wakaenda wakaniambia, Chukua. Killa endapo ikawa kazi ni hiyo. Lete paa, hupeleka wakatezama, Ahh! bassi, ghali, chukua. Nami hichukua. Huondoka nikienda mbele, Ewe muhadimu, ewe lete paa, lete. Nami hupeleka, nikatua wakatazama. Ah! paa wazuri, lakini ghali, chukua paa. Nami hichukua, nami nisikasirike, ni ada ya mchukua biashara ya kwitwa hapa na hapa, na kutua na kujitwika, nami nisikasirike, kwani ni ada ya biashara, humjui atakayonunua, wewe hunena, labuda huyu atanunua, huyu atanunua, hatta upate mnunuzi hatta kununua.

Bassi wewe maneno yetu huyashiki, umetolewa wingi wa maneno na wingi wa masaala, enenda zako maskini.

Bassi wale wakanena wale watu watatu, 'M! Bassi nasi tutamfuata, kamtazame yule maskini, atanunua kweli.

Ee, bwana, apate wapi yule? Maneno gani hayo? 'M! dalili za kupata mtu hazionekani. 'M! tokea kufa mkewe, yule akatoa mali yake akafanya uasherati, haipungui mwaka wa tatu, hajui chakula cha moto tumboni mwake. Bassi mtu asioweza kupata chakula cha moto tumboni