Page:Swahili tales.djvu/70

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
50
SULTANI DARAI.

Akamwambia, mimi sina kasarani kwenu, napenda killa siku mje kwa killa wakati, mje nimtazame nami mwanangu huyu mmoja, sipendi kumkosa sana. Akamwambia, Inshallah, bwana.

Hatta jua lalipokuchwa wakihama yeye na mkewe, wakaenda zao kwake. Wakakaa sana na yule mwanamke, wakapendana sana. Na yule mwanamke akampenda sana mumewe, mapendo asiokuwa na kifani. Ampenda sana mkwewe yule mwanamume, asiokuwa na kifani.

Wakakaa miaka mingi, wasigombe yeye na mkewe, wala wasigombe yeye na mkwewe. Wakakaa watu hawa, mashauri yao mamoja, hatta yule mkwewe akapatikana na farathi akafa. Wakasimama, yeye na mkewe, wakamzika.

Wakakaa muda ya miaka mingi kupita, akapatikana na farathi mkewe, akafa, akasimama akamzika.

Bassi akakaa kitako yeye pekeyake, akakaa muda ya siku nyingi kupita, akafanya mambo ya asherati, killa alichonacho kikampotea, kwa uasherati mwingi.

Akakaa mtu wa kuomba, killa nyumba huenda akiomba, akipata. Akapita siku zile, nyumba alizo akaenda akiomba, asipewe kitu tena. Akaregea katika jaa, akapekua kama kuku, akipata punje za mtama, akitwaa akila, muda ya siku nyingi.

Hatta siku hiyo, akienda jaani akaenda akipekua, akapata themuni ya mzinga, akainama marra ya pili, akapekua jaani, asipate hatta punje moja ya mtama. Ahh! mimi nimepata themuni hii ya mzinga, bassi ntakwenda zangu, nikalale. Akaenda hatta nyumbani, akatwaa maji, akanywa, akatwaa na tumbako, akatafuna. Ndicho kitu