Page:Swahili tales.djvu/64

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
44
SULTANI DARAI.

Bassi yeye yu tayari, fanye nawe yako shauri. Akamwambia, mimi sina shauri, shauri yangu imekwisha, ni kukupa nguo, na mahari, na mkaja, na kilemba, na ubeleko.

Bassi nipe upesi, nipeleke kabla jua halijachwa. Akamwambia, zote tayari, nimekwisha kuziweka, nalikungoja wewe kutwaa, na wewe wazitaka, tayari. Ingie ndani kanipe upesi, nami nna shughuli, ntakwenda zangu.

Mwanamume akaingia ndani, akaenda akatwaa mahari, akaenda akatwaa kilemba, akaenda akatwaa mkaja, akaenda akatwaa ubeleko. Akaisha akamwambia, na kiosha miguu, chukua, na kifungua mwango, chukua. Akamwambia kipa mkono ntachukua mwenyewe. Bassi nawe enenda uwapelekee na salaam, mimi huku ni tayari, nangoja wao waje waniite.

Akatoka akachukua zote alizopewa, akaenda hatta kwa babaye yule mke, hako, akamwambia mkewe, kendapi huyu mumeo? Ametwambia anazunguka nyuma kwa jirani, kwenda kucheza tiabu, alitwagiza, uje hapo tume, mtoto akamwite.

Akanena, bassi upesi, kaniitieni, nami hapa namngoja. Akaondoka mtoto, akaenda mbio hatta pale nyuma kwa jirani, akamwona babaye anacheza tiabu, akampungia mkono kumwita. Babaye akatambua, akawaambia, Mimi naondoka jamaa, akaja mtoto kuniita, labuda nyumbani kuna shughuli. Wakamwambia, Haya, enenda.

Akaenda hatta kwake, akamwona tume wake anamngoja barazani, Je! umekuja. Amwambia, nimekuja, bwana. Habari za utokako? Akamwambia, Habari za nitokako njema sana, tena za kufurahisha, tena za kupendeza, amana yako imekuja, ya kwanza hii mahari, za pili hizi