Page:Swahili tales.djvu/56

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
36
SULTANI DARAI.

kwako, baba yangu, yule mama kusikia hatanipenda. Atanambia, yule mwana si kitu, ananiacha kuniomba mimi mamaye, shuti akamwombe baba yake, bassi mimi mke wa nini nyumbani?

Akamwambia, kweli mwanangu. Bassi nipe habari ya tango hili, mwanangu.

Akamwambia, tango lile naliokuja nalo juzi, siku ile ulipokuwa hawezi, walipokwenda kwenda kwa jirani kwenda kucheza bao, ukarudi upesi, kabla mtu hajaja kukwita, ukamwuliza mama, mbona kimekawia, jua limekuwa mafungulia ng'ombe, hakukwambia chakula kimekwisha, nali nikiosha sahani, nipate kumtuma mtu, aje akwite? Ukamwambia, kama chakula kimekwisha, pakue. Akamwambia, kimekwisha, akaenda akapakua mwanamke sahani tatu, moja yako baba, moja ya mwanawe, moja yangu. Sahani yako ya wali, naye mwanawe ya wali, yangu mimi imetiwa ukoko tena ulioungua, na kitwa cha samaki. Wangu nikazunguka nao nyuma, hautazama ule wali siwezi kula, nikasikitika sana, nikalia sana, nikanena na mimi mama yangu angekuwa hayi, ningekula wali mwema na mimi, kama anavyokula mwenzangu, anavyopewa na mamaye. Bassi walipokwisha kula wewe baba, waliponawa mkono wakatoka, na mimi nikatoka kwa uchungu wa roho yangu, nikaenda hatta kaburini kwa mama yangu, nikasikitika sana, nikalia sana, tena nikaondoka nikazunguka nyuma ya kaburi, hatazama chini, haona mtango, hachuma matango mawili, moja hatafuna, na moja hachukua mwenyewe kufanya mtoto. Nalipokuja hapa nyumbani, huyu mama akaniuliza, watoka wapi na tango? Mimi simwambii, natoka nalo kaburini kwa mama yangu, nika-