Page:Swahili tales.djvu/50

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
30
SULTANI DARAI.

nipakue? Kama u tayari, pakua. Akaenda akaingia jikoni mwanamke, akipakua sahani tatu, sahani moja ya mumewe, sahani moja ya mtoto wa mumewe, na sahani moja ya mwanawe. Na sahani mbili zile za wali mwema, sahani ya mumewe na sahani ya mwanawe, na sahani ya yule mtoto wa mumewe ametia ukoko wa wali, na ukoko umeungua, na kitwa cha samaki, ndicho alichompa. Mumewe akapelekewa wali, na mwanawe akachukua wake wali, na mtoto wa mumewe akachukua ukoko ule ulioungua. Na yule mume roho yake inasikitika kwa sababu hapati kula na mwanawe sahani moja, na kunena kwa yule mwanamke hathubutu.

Akamwambia, bibi, watoto wamekula? Akamwambia, nimekwisha wapa sahemu zao, wamekula yee na nduguye. Akamwambia, bass, nipe maji ninawe, na akinawa mkono, mume akatoka.

Na yule mtoto wake kule nyuma aliko hakula ule wali, analia, anasikitika kuona mwenziwe ana mwema, naye kula ukoko. Akiacha ule ukoko, akaenda hatta kaburini kwa mama, akaenda akisikitika sana, na kulia sana.

Akizunguka katika nyuma ya kaburi, akaona mtango. Akatazama chini, akaona matango, akichuma mawili, moja akila, moja akachukua kufanya mtoto. Hatta alipofika kule nyumbani. Tango hili umepata api? Akamwambia, tango hili nimechuma kule shambani kwa watu. Akamwambia, nilete tango. Akamnyang'anya, akimpa mwanawe. Yule akakaa kitako akilia.

Hatta babaye alipotoka, amkuta kijana analia. Je! mama, unalilia nini? Akamwambia, sina hatta kitu. Unalia burre? Una jawabu ndani ya roho yako, nambie