Page:Swahili tales.djvu/496

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
476
UTUMBUIZO WA GUNGU.


Mwangalie usita wa yumbe,
Ao kwao kwa fumo wa ezi,
Mwangalie tengoni pa uduze,
Ao kwao kwa mama shangazi,
Kampate, hima uye naye.
Watendani hatta njeu shizi
Kamwambia, bwana, waamknwa,
Tenda hima, sifanye ajizi,
Yanga lako wimie tutule,
Na matoni hutuza tozi.
Kaamba tende tangulia, naja,
Kamtuze, ate simanzi,
Kamwandama nyuma kiongoya,
Akinuka meski na mbazi.
Akiingia kampa salamu,
Kamjibu mwana wa Hejazi.
Saa hiyo kaondoka akaima,
Kamwaudika mkono wa fuzi,
Kamwombea Muimgu Jabari,
Ewe mama, Mola ngwakujazi.




Mtezame njia ya Sultani,
Ao kwao wa mfahne aliyetawala,
Mtezame vikaoni vya nduguze,
Ao kwao kwa mamaye, shangazi Lake,
Kamshike, upesi uje naye,
Wafanya nini hatta wakati huu?
Kamwambia, Bwana, unakwitwa,
Twendo npesi, sifanye uvivu,
Kukawilia kwako huchoka kusimama
Na machoni yatoka machozi.