Jump to content

Page:Swahili tales.djvu/468

From Wikisource
This page has been proofread.
448
HADITHI YA LIONGO.

mkoma akaangue, tule, tukiisha apande mgine, hatta tuishe. Akawaambia, vema.

Akapanda wa kwanza, wakala. Akapanda wa pili, wakala. Akapanda wa tatu, wakala. Na wale wamefanya hila, atakapopanda Liongo tumpige kwa mishare kulekule juu.

Liongo akatambua kwa akili yake. Hatta walipokwisha wote, wakamwambia, haya, zamu yako. Akawaambia, vema. Akashika mkononi uta wake na viembe, akawaambia—

Tafuma wivu la angania, tule cha yayi.

Maana yake, Nitapiga bivu la juu tule cha kati. Akapiga, likakatika tawi, akapiga tena, likakatika la pili, akaupukusa mkoma mzima, yakajaa tele chini. Wakala. Hatta walipokwisha, wale watu wakasema wao kwa wao, ametambua huyu, sasa tufanyeje? Wakanena, twendeni zetu. Wale wakamwaga, wakamwambia—

Kukuingia hadaani Liongo fumo si mtu,
Yunga jini Liongo okoka.

Maana yake, Hukuingia ujingani, Liongo mfalme, wewe si mtu, kamma Sheitani umeokoka.

Wakaenda zao, wakajibu kwa yule mkuu wao, alioko mjini, wakamwambia, hatukuweza.

Wakafanya mashauri—nani atakayeweza ku'mua? Wakanena, labuda mtoto wa nduguye. "Wakaenda wakamwita. Akaja. Wakamwambia, enenda, kamwuliza babayo, kitu gani kinachomwua, ukiisha kujua, uje utwa-