Page:Swahili tales.djvu/466

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
446
HADITHI YA LIONGO.

pige. Akawaambia, mmoja ashike pembe, na mmoja ashike matoazi, na mmoja ashike upato. Wakamwambia, tupigeje? Akawafundisha kupiga, wakapiga.

Naye mwenyewe ndani kule aliko akaimba, hatta ilipositawi ngoma, akashika tupa, akakata pingu. Ile ngoma ikinyamaa naye bunyamaa, akaimba, wakipiga, yeye akakata pingu.

Na watu wale hawana khabari ilioko ndani, hatta ikakatika pingu, akakata na mnyororo hatta ukakatika. Na wale watu hawana khabari kwa shanko ya ngoma. Wakitahamaka amevunja mlango amewatokea nje. Wakitupa vitu hivi kwenda mbio wasidiriki, akawakamata akawapiga vitwa kwa vitwa akiwaua. Akitokea nje ya mji, akaagana na mamaye, kutuonana tena.

Akaenda zake mwituni akakaa kitako siku nyingi huuthi watu vilevile na kuwaua watu.

Wakatuma watu wa hila, wakawaambia, enendi, mkafanya rafiki hatta mmwue. Wale wakaenda wa khofu. Walipofika wakafanya urafiki, Hatta siku hiyo wakamwambia, tule kikoa, Sultani. Yeye Liongo akawajibu—

Hila kikoa halipani nikatamno?

Maana yake—Nikila kikoa nitalipa nini, masikini mno? Wakamwambia, tule kikoa cha makoma. Akawauliza, tutakulaje? Wakamwambia, atapanda mtu mmoja juu ya