Page:Swahili tales.djvu/462

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
442
HADITHI YA LIONGO.

usiku usiku, kuimba nyimbo nzuri, kulla asikiaye huzipenda sana zile nyimbo. Kulla mtu humwambia rafiki yake, twende tukasikilize nyimbo za Liongo, anazokwimba chumbani. Huenenda, wakisikiliza. Kulla siku ikipata usiku, huenda watu, wakamwambia, tumekuja kwimba nyimbo zako, tusikie. Huimba, hawezi kukataa, wakazipenda mno watu mjini. Na kulla siku kutunga nyingine nyingine kwa sikitiko la kufungwa. Hatta watu wamezijua nyimbo zile kidogo kidogo, lakini yeye, na mamaye, na mtumwa wake wanazijua sana. Na maana yake zile nyimbo mamaye azijua, na wale watu mjini hawajui maana yake.

Hatta siku hiyo kijakazi chao ameleta chakula wakamnyang'anya wale asikari, wakala, wakamsazia makombo, wakampa. Yule kijakazi akamwambia bwana wake, nimeleta chakula, wameninyang'anya hawa asikari, wamekula, wamesaza haya makombo. Akamwambia, nipe. Akapokea, akala, akashukuru Muungu kwa yale yaliompata.

Akamwambia kijakazi chake (na yeye ndani na kijakazi yu nje ya mlango)

Ewe kijakazi nakutuma uwatumika,
Kamwambia mama, ni mwinga siyalimka.
Afanye mkate, pale kati tupa kaweka,
Nikeze pingu na minyoo ikinyoka,
Ningie ondoni ninyinyirike ja mana nyoka,
Tatange madari na makuta kuno kimeta.

Maana yake—Wee kijakazi utatumika kamwambia mama, ni mjinga sijaerevuka, afanye mkate, katikati aweke tupa nikate pingu, na minyololo ikifunguka, niingie njiani,