Page:Swahili tales.djvu/46

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
26
SULTANI DARAI.

Chakula kimekwisha. Oh! kimekwisha zamani, bwana, tena wali umepoa. Pakua upesi, nataka kulala.

Mwanamke akaenda jikoni, akapakua wali upesi, akaja akamwandikia mumewe. Akaleta maji ya kunawa. Mumewe akanawa mkono. Akamwambia, waite watoto tupate kula chakula.

Ah! mume wangu huna mashikio? Maneno yayo kwa yayo sikuzote, ela vijana wakae kitako na chakula kimekwisha wakungojea wewe hatta urudipo kazini, saa ya saba? Watoto hawa wangekufa na njaa, lakini miye hupika upesi makusudi, hawa vijana wale na mapema, wasione njaa. Bassi wewe, killa siku unaporudi kazini, huwaite watoto ule nao, wataka kuwalisha marra mbili ao tatu hawa, bassi hayo mambo gani?

Ee bibi sina habari, kama watoto wamekwisha kula, bassi bibi, ningekuwa na habari ningewaita marra ya pili? Lakini nnanena, hawajala, ndio maana hawaita, sasa wamekula, bass! Kanawe, tule.

Na mwanamke akaenda kunawa, wakarudi, wakala. Akamwambia, desturi, mume wangu, ujapo uje shuti waite watoto, huwaambia watoto njooni mle, na desturi za nyumba kwanza huulizwa mke, kwani ndiyo alionao nyumbani, kwani ndiye ajuaye vitu pia vipikwavyo na vibichi, na ashibaye na mwenyi njaa, kwani mke ndiye ajuaye, kwani yee ndiye mpishi, ndiye apakuaye, bassi ukija, mume wangu, sasa desturi ukiniuliza mimi, kwani ndiyo ulioniachia nyumba yako kwani nasikia, ndio mkeo mimi.

Bassi, mke wangu, uwe rathi kwa hili nalionena, na hili nalilokosa, haya walioniambia ndio maneno ya sheria ya