Page:Swahili tales.djvu/448

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
428
NYANI, NA SIMBA, NA NYOKA.

mkuu na nyika kuu, akaenenda wakaonana na lile nyani. Yule bin Adamu akaulizwa habari ni nyani. Akamwuliza, Ewe bin Adamu, wenda api? Akamwambia kwamba nimepotea. Akamwambia, bwaga moyo hapa, mimi nikulipe leo yale mema yako uliyotendea juzi, ukanitoa katika mtego, bassi starehe uningoje hapa.

Akaenenda nyani hatta mashambani mwa watu, akaenda akaiba mapapai mabivu, akaiba na ndizi mbivu, akamchukulia yule bin Adamu, akamwambia, twaa vyakula hivi, ndizi na mapapai, akampa yule bin Adamu. Akamwambia, watakani, wataka maji? Akaenda akaiba kibuyu kya maji akampa bin Adamu akanywa, akaisha kunywa, wakaagana. Wakawaambia, kua heri, kua heri ya kuonana. Akaenda zakwe.

Alipofika kule mbele, akaenenda, wakakutana na simba. Alipokutana akamwambia simba, watoka wapi, bin Adamu? Yule bin Adamu akamwambia simba, nimepotea. Simba akamwambia, kaa kitako hapa, nikulipe yale mema yako ya juzi ulionifaa, nami nikufale, kaa hapa. Akastarehe bin Adamu, akamsaburi simba. Simba yule akaenda akakamata nyama, akamletea bin Adamu, akasema, umepotea, vyakula hivi la, nije 'lipe yale mema yako ya juzi. Akampa nyama na moto wa kuoka nyama. Akaoka nyama akala. Alipokwisha kula nyama akatawakali, akaenda zakwe bin Adamu.

Alipokwenda zakwe bin Adamu akaenda akatokea shamba, pana mwanamke shaibu la juza, akatokea mtu pale, akamwambia, huko mjini kwetu kuna mtu amehawezi,