Page:Swahili tales.djvu/424

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
404
AO RATHI, AO MALI.

tana hatta njiani wakaona ziwa kubwa. Nyoka akamwambia, mwana Adamii, tukae tupumzike, jua kali, enenda kaoge ziwani na mtoto. Akamchukua kijana chake, akaenda kumwosha, akatumbukia, akampotea ziwani. Akamwuliza, una nini, mwana Adamu, huko? Akamwambia, mtoto wangu amepotea ndani ya maji. Akamwambia, mtafute sana. Akamtafuta saa mzima, asimwone. Akamwambia, tia mkono wa pili. Akamwambia, weye nyoka unanifanyia mzaha. Akamwuliza, kwa nini? Akamwambia, nimetia huu mzima, sikumwona, huu mbovu utafaa nini? Nyoka akamwambia, tia tu weye yote miwili. Akatia mwana Adamu, akaenda akamwona mwanawe, akamshika, akimtoa mkono wake mzima. Akamwambia, umemwona? Akamwambia, nimemwona na mkono wangu nimepata mzima. Akafurahi sana.

Akamwambia nyoka, sasa twende zetu kwa wazee wangu, nikakulipe fathali huko. Akamwambia, hii yatosha, kupata mkono wangu. Akamwambia, bado, twende wazee wangu. Wakaenda hatta walipofika, wakafurahi sana, wakampenda yule kijana manamke. Akakaa kitako, akila, na kulala, siku nyingi.

Yule mumewe akarudi kutembea. Wale wazee wake wakafanyiza makaburi mawili, moja la mkewe, na moja la mtoto wake. Na yule ndugu yako manamume amekua mtu mkubwa kwa mfalme.

Akaja mumewe kijana cha mfalme. Akauliza, mke wangu yu wapi? Wakamwambia, amekufa. Na mtoto wangu yu wapi? Wakamjibu, amekufa. Akauliza, makaburi yao yako wapi? Wakampeleka kuenda kuyaona.