Page:Swahili tales.djvu/422

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
402
AO RATHI, AO MALI.

ameoa manamke, hana mkono moja. Yule nduguye manamume akauliza, amempata wapi kijana huyu mtoto wa mfalme? Wakamwambia, amemwokota mwituni. Akamjua kuwa nduguye.

Akaenda hatta kwa mfalme. Akaenda akamwambia, mtoto wako ameoa manamke hana mkono moja, ametolewa huyu katika mji wao kwa sababu mchawi, killa mume anayemwoa humwua.

Na mfalme akaenda akamwambia mkewe, wakanena, kufanya shauri gani? Nao wanampenda sana mtoto wao mmoja tu, wakasema, kumtoa mji yule. Nduguye mwanamume akawaambia, mwueni, kwani huko kwao amekatwa mkono, na hapa mwueni. "Wakamwambia, hatuwezi kumwua, tutamtoa mji. Wakaenda, wakamtoa mji, yeye na mwanawe. Akashukuru Muungu.

Akatoka, amechukua kitunga, akaenda zake, hatta mwituni, hajui anapokwenda, wala anakotoka. Akakaa kitako, akamwonyesha manawe, akitupa macho, akaona, nyoka anakuja mbio hatta karibu yake, akanena, leo nimekufa.

Nyoka akamwambia, mwana Adamu, funua kitunga chako niingie, uniponye wa jua nitakuponya wa mvua. Akafunua akaingia, akafunika. Akitezama, akaona nyoka mgine anakuja mbio, akamwambia, hakupita mwenzangu? Akamwambia, huyu anakwenda. Akapita mbio.

Yule nyoka, aliomo kitungani, akamwambia, nifunua. Akamfunua, akashukuru Muungu, akamwambia yule mwana Adamu, unakwenda wapi weye? Akamwambia, sijui ninapokwenda, ninapotea katika mwitu. Akamwambia nyoka, fuata mimi, twende kwetu. Wakafua-