Jump to content

Page:Swahili tales.djvu/418

From Wikisource
This page has been proofread.
398
AO RATHI, AO MALI.

Yule akapotea na mwitu, hatta siku ya saba akatokea mji mgine. Akapanda juu yamti mkubwa, akila matunda ya mti, usiku hulala mle mtini. Hatta siku ya pili, akatokea kijana cha mfalme anapiga ndege, yee na watu wake. Hatta saa ya sita amechoka, asema, nitakwenda pale mtini, nikapumzike, na ninyi pigeni ndege. Akakaa chini ya mti, yee na mtumwa wake.

Yule kijana manamke akalia hatta machozi yakamwangukia mtoto wa mfalme chini. Akamwambia mtumwa wake, angalia nje, hakuna mvua? Akamwambia, hakuna, bwana. Akamwambia, bassi, panda mtini uangalie ndege gani alionitia mavi. Akapanda mtumwa wake, akamwona manamke mzuri mno analia, asimwambie neno, akashuka. Akamwambia bwana wake, kuna kijana manamke mzuri mno, sikuthubutu kumwambia neno. Bwana wake akamwuliza, kwa nini? Akamwambia, nimemkuta, analia, labuda wende wewe. Akapanda bwana wake, akaenda, akamwona, akamwambia, una nini, bibi yangu, weye mtu, ao pepo? Akamwambia, mimi mtu. Akamwambia, unalilia nini? Akamwambia, nakumbuka ulimwengu, mimi ni mtu kana wewe.

Akamwambia, shuka, twende zetu kwetu. Akamwambia, kwenu wapi? Akamwambia, kwa baba yangu na mama yangu, mimi ni kijana cha mfalme. Akamwambia, umekuja fanya nini huku? Akamwambia, nimekuja kupiga ndege, mwezi hatta mwezi ndio kazi yetu, nimekuja na wenzangu wengi. Akamwambia, mimi sitaki kuonekana na mtu. Yule manamke, amemwambia kijana cha mfalme. Akamwambia, hatuonekani na mtu. Akashuka chini.

Akamtuma mtumwa wake—enenda mjini upesi, uka-