Page:Swahili tales.djvu/416

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
396
AO RATHI, AO MALI.

mtumwa wake na nafaka kuenda kumnunulia boga. Akamwambia, yamekwisha. Alipojua mtumwa yule wa mke wa nduguye, akamwambia, twaa ile moja, mpelekee, na nafaka yako rudi nayo. Akaenda akalipika, akaona tamu mno. Siku ya pili akampeleka tena mtu. Akamwambia, hapana kabisa leo. Akaenda, akamjibu bibi yake, akakasirika mno.

Hatta mumewe alipokuja, akamwuuza, una nini mke wangu? Akamwambia, nimepeleka mtu kwa ndugu yako na nafaka yangu, kuenda kutaka maboga, hakuniletea, ameniambia, hakuna, na watu wote hununua kwake! Akamwambia mkewe, na tulale hatta kesho nitakwenda kung'oa mboga wake.

Hatta subui kukicha akaenenda kwa nduguye, akamwambia, mke wangu kuleta nafaka ukakataa kumliza boga. Akamwambia, yamekwisha, jana alileta mtu, nikampa burre. Akamwambia, mbona watu unawaliza? Akamwambia, yamekwisha, hakuna tena, hayajazaa. Ndugu yake manamume akamwambia, nitakwenda ukata mboga wako. Akamwambia, huthubutu, labuda ukate mkono wangu kwanza, ndipo mboga uukate. Ndugu yake akakamata mkono wake wa kuume, akamkata, akaenda akaukata na mboga wote pia.

Yule manamke akateleka maji ya moto, akatia mkono wake, akatia na dawa, akafunga kitambaa.

Akamnyang'anya vitu vyote, akamtoa na nyumba.

Akapotea yule nduguye ndani ya mwitu. Nduguye huyu akauza nyumba, akakusanya mali mengi, akakaa akitumia.