Page:Swahili tales.djvu/408

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
388
PEPO NA MTOTO WA SULTANI.

kuja kutembea. Wakaenda wakamwambia mfalme, amekuja kutembea mgeni. Akawaambia, enendo mtu kesho amwambie, Sultani atakuja kukutezama. Akaenda mtu, akamwambia. Akamwambia, marahaba na aje.

Akaamrisha kufanya vyakula vingi. Hatta assubui mfalme akaenda, na watu wake, akafika nyumbani. Akamkaribisha, akapita ndani, akaona Sultani nyumba kubwa na watumwa wengi ndani. Akakaa kitako, wakazumgumza. Akamwuliza, kwa nini huji mjini kutembea? Akamwambia, mimi mgeni, sharti nipate watu wanitwae, wanipeleke mjini. Akamwambia, twende zetu, tukatembee.

Mfalme akampenda sana, wakakaa siku nyingi pale. Mfalme akamwuliza, utake mke kuoa? Akamwambia, nataka. Akamwambia, nitakuoza mwanangu. Akafanya harusi kubwa Sultani akamwoza.

Akakaa na mkewe, akazaa mtoto mmoja, wakakaa hatta hatima, yee na mkewe na mtoto wake mmoja, na frasi yake, akampenda kama roho yake.