Page:Swahili tales.djvu/406

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
386
PEPO NA MTOTO WA SULTANI.

Akamwambia, panda mwenyewe kwanza, ucheze, nami nikiona baba, nipate kucheza. Akapanda, akacheza. Akashika, akamsukuma ndani ya sufuria, akatokota pamoja na samli, akafa.

Akakimbia mtoto, akaenda hatta chini ya mti akaona farasi akaja mbio. Farasi akaja, akamkamata, aka'mweka juu ya maungo yake, akamwambia, twende zetu sasa. Wakaenda zao.

Wale wenziwe kule wakaja, wakamtafuta, hawamwoni. Na njaa inawauma sana, wakaangalia ndani ya sufuria wakaona chakula kimekwisha, wakasema, katule chakula hiki, wakaepua wakapakua, wakala. Hatta walipokwisha, wakamtafuta, hawamwoni. Wakaingia ndani ya nyumba, wakatoa vyakula pia na michele pia, wakaja wakapika, wakala, siku ya pili tena, wakaona hajaja, wakaenda zao kwao.

Huyu mtoto, yee na farasi wakaenda hatta mbali miji mingine, wakakaa mwisho wa mji. Akamwambia, hapa tukae, wakakaa, wakala chakula. Akamwambia, hapa, tujenge nyumba, wakajenga nyumba kubwa na killa kitu ndani, wakatia punda na farasi na ng'ombe na mbuzi na watumwa, wakakaa.

Hatta siku yule Sultani akasikia, akaenda, akapeleka watu, wakaenda kutezama kweli habari iko nyumba kubwa, watu waambia, kweli Sultani, ni nyumba kubwa.

Sultani akampelekea watu wake kuangalia nani huyu. Akawaambia, mimi mtu kama watu. Wakamwambia, watoka wapi? Akawaambia, natoka mjini kwetu, nime-