Page:Swahili tales.djvu/400

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.

PEPO ALIYEDANGANYWA NA MTOTO WA SULTANI.


Palikuwa na Sultani akitamani kijana siku nyingi, asipate. Naye ana mali mengi na miji mingi. Akaona—nikifa, itapotea mulki huu pia kwa sababu ya kukosa mtoto.

Akaja sheitani akajifanya kama mtu, akamwambia Sultani, nikikupa dawa, ukipata mtoto, utanipa nini? Akamwambia, nitakupa nussu ya mali yangu. Akamwambia, sitakubali. Akamwambia, nitakupa miji yangu nussu. Akamwambia, sikubali. Akamwambia, wataka nini bass? Akamwambia, ukizaa watoto wawili, nipe mmoja, nawe utwas mmoja. Akamwambia, nimekubali.

Akamletea dawa, akamwambia, mpe mkewo, ale. Akampa, akala, akachukua mimba, akazaa mtoto wa kwanza manamume, na wa pili manamume, na wa tatu tena manamume.

Akaja rafiki yake yule aliompa dawa, akamwambia—haya, tugawanye. Akamwambia, bado, hawajasoma watoto hawa. Akamwambia nipe mimi nikawasomeshe, akamwa-