Page:Swahili tales.djvu/396

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
376
SUNGURA NA SIMBA.

Akarudi taratibu, akaenda akasimama mbali, akatoa salaamu, akasema—Salaam nyumba! Salaam nyumba! Salaamu nyumba! Akasikia kimya. Akanena sungura, gissi gani killa siku nikipita hapa, nikitoa salaamu, nyumba hunijibu, labuda leo mna mtu humo ndani. Yule simba akadanganika, akaitikia—Salaamu!

Akamwambia—Looo! simba umo ndani, wataka kunila mimi mwanao, ukasikia wapi nyumba kusema? Simba akamwambia, uningoje bass. Sungura akakimbia, wakafukuzana hatta simba akachoka. Akawaambia watu, sungura akanishinda, bass, simtaki tena. Akarudi.