Page:Swahili tales.djvu/392

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
372
SUNGURA NA SIMBA.

Simba akamwambia, shuka bassi. Akashuka. Akamkamata, akamwambia, walikuwa weye na nani huko juu? Akamwambia, mimi na sungura. Hukumwona hapa nalipomtupa? Akamwambia, sikumwona. Akamla buku. Simba akatoka kuenda kumtafuta sungura, asimwone.

Hatta siku ya tatu sungura akaenda, akamwita kobe, akamwambia, twende, tukale asali. Akamwuliza—ya nani? Akamwambia, ya baba yangu. Akamwambia, twende. Wakafika, wakapanda juu na mienge yao ya moto, wakachoma nyuki, wakakimbia, wakakaa kitako, wakala.

Marra akatokea simba, na yule simba ndio mwenyewe asali. Akawauliza, nani ninyi juu? Sungura akamwambia kobe, nyamaza. Akauliza tena simba. Kobe akaogopa, akamwambia, mimi nitasema, umeniambia asali hii yako, kumbe si yako, ya mwenyewe simba? Simba akauliza tena, nani ninyi? Akamwambia, sisi hapa. Akawaambia, shukeni bass. Akamwambia, tunakuja. Na simba akamtafuta sungura siku nyingi, akasema, leo nitapata sungura.

Sungura akamwambia kobe, unitwae mimi unitie ndani ya mwenge, umwambie simba, jitenge nitupe mwenge, nami nitakwenda, uningoje chini. Akamwambia—Vema. Kobe akasema moyoni mwake, huyu ataka kukimbia, kuniacha mimi niliwe na simba, ataliwa yee mbele. Akamtwaa akamtia ndani ya mwenge. Akamwambia simba, Sungura huyu anakuja.

Simba akamdaka, akamkamata mkononi, akamwambia, nikufanyeje leo? Akamwambia, ukinila nyama yangu