Page:Swahili tales.djvu/378

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
358
HASSIBU KARIM AD DINI.

akaenda kuoga. Hatta akitoka, amekufa, nikamzika hapa. Wale Majini wakaenda kwa babaye kumwambia, mwanawo amekufa. Babaye akasema, kamwiteni Jani Shah, aje, aoe huyu mtoto mgine. Wakaja kuniambia. Nimesema, sitaki, nitachimba kaburi la pili, nikifa, niingie ndani. Ndio kisa changu.

Akakaa hatta akafa. Na yule Bolukia akaenda zake, akafa njiani.

Sultani wa nyoka akamwambia Hassibu, na wewe ukienda kwenu utanifanya vibaya. Akamwambia, sitakufanya vibaya, nipeleke kwetu. Akamwambia, miye najua, nikikupeleka kwenu, utarudi, uje, uniue. Akamwambia, sithubutu, nipe kiapo, niape. Akampa watu, wakampeleka kwao. Akamwambia, ukifika kwenu, usiende kuoga panapo watu wengi. Akamwambia, siendi. Wakampeleka kwao, hatta walipofika, wakarudi wale, wakamwambia, kua heri. Akaenda kwa mamaye, akafurahi sana mamaye.

Na mle mjini mwao, Sultani hawezi sana, na dawa yake sharuti apatikane Sultani wa nyoka, auawe, nyama yake itokoswe, ndio dawa.

Yule waziri akaweka watu katika hamami, akawaambia, akija mtu kuoga ana alama tumboni mkamateni.

Yule Hassibu akakaa siku tatu, akasahau maneno ya yule rafiki yake Sultani wa nyoka, akaenda kuoga.

Wale asikari wakamkamata, wakampeleka kwa waziri. Waziri akamwambia, utupeleke mahala alipokaa Sultani wa nyoka. Akamwambia, sipajui. Akawaambia, mfungeni. Akafungwa akapigwa sana, akapasukapasuka maongoni. Akawaambia, nifungueni, niwapeleke.