Page:Swahili tales.djvu/374

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
354
HASSIBU KARIM AD DINI.

Nikasema, nimekufa mimi. Nikaenenda mwituni siku nyingi. Nikatokea nyumba moja, nikamwona mzee katika nyumba, akanipa chakula na maji, nikashukuru Muungu.

Nikakaa kitako pale, akanipenda kana mwanawe. Akanipa funguo zote za nyumba, akaniambia, fungua kulla utakapo, ela chumba hiki kimoja usifungue. Nikamwambia, vema, baba.

Nikakaa, akatoka yee kwenda kutembea, nikafungua mimi, nikaona bustani kubwa, na mto unapita. Marra wakaja ndege watatu, wakatua pale mtoni. Marra wakageuka watu, wakaoga mtoni, na wazuri mno wale watatu waanawake. Nikawatezama hatta walipokwisha kuoga, wakavaa nguo zao, wakaruka.

Nikarudi mimi, nikafunga mlango, nisiweze kula kitu. Hatta baba yangu akaja, akaniuliza, una nini? Nikamwambia, nimekwenda katika bustani, nimeona waanawake watatu, wamekuja kuoga, wamekwisha, wameruka, na yule mmoja nampenda mno, nataka kumwoa, kama sikumpata nitakufa.

Akaniambia, wale hawapatikani, wale watoto wa Sultani wa majini, na kwao mbali sana, mwendo miaka mitatu. Nikamwambia, sijui, sharti unipatie. Akaniambia, ngoja marra hii, watakapokuja kuoga, ujifiche, utwae nguo za yule umpendaye sana.

Nikaenda nikangoja, hatta walipokuja wakavua nguo zao, nikazitwaa, nikazificha. Na yule ndio mdogo wao, na jina lake Seyedati Shemsi. Walipotoka wakavaa nguo zao, wale nduguze, yee akatafuta zake, asizione. Nika-