Page:Swahili tales.djvu/372

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
352
HASSIBU KARIM AD DINI.

kubwa ya mawe, na mlango wakwe umeandikwa. Nikasoma mimi, ya kwamba, mtu anaokuja hapa kisiwani, hawa kima hawamwachi kumpenda mno mfanya ndio mfalme wao. Na atakapokwenda zake, hapati njia, lakini iko njia moja, imelekea kibula, hufuata njia hiyo, hutaona uwanja mkubwa, una simba na chui na nyoka, mtapigana nao, mkiwashinda, mtapata njia, mtakwenda mbele, mtaona uwanja mgine, una tungu wakubwa, kana mbwa, na meno yao kana mbwa, wakali sana, mtapigana nao, mkiwashinda, mtapata njia ya kupita.

Tukafanya mashauri, wale watumwa wangu wakaniambia, tuenende, tukapone ao tukafe, na sisi sote tuna selaha zetu.

Tukaenenda hatta tukafika uwanja wa kwanza, tukapigana, wakafa watumwa wangu wawili. Tukaenda zetu, tukapita, tukaenda wa pili, tukapigana, wakafa watumwa wangu wawili, nikapona mimi.

Nikapotea siku nyingi, hatta nikatokea mji. Nikakaa kitako pale mjini, nnatafuta kazi, sipati. Akatokea mtu, akaniambia, wataka kazi? Nikamwambia, nataka. Akaniambia, twende zetu, tukaenda kwake.

Akachinja ngamia, akatwaa ngozi ile, akaniambia, nitakutia ndani ya ngozi, wende juu ya jabali, ndege atakuchukua, ukifika atakufungua, usukume vito chini, ukiisha nitakushusha mimi.

Akanitia ngozi ile, akaja ndege, akanichukua akaniweka juu ya jabali, akataka kunila, nikaondoka, nikamfukuza ndege, akaruka. Nikasukuma vito chini vingi, nikamwambia, nishushe, bass! Asinijibu neno, akaenda zake.