Page:Swahili tales.djvu/370

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
350
HASSIBU KARIM AD DINI.

twalimfukuza paa, hatta tukafika pwani, yule paa akaingia baharini, wakaingia mashuani, yee bwana na watu wanne, wakamfukuza, sisi tukarudi.

Baba yangu akasema, mwanangu amekwisha potea. Akaenda zake mjini, akakaa matanga, akashukuru Muungu.

Sisi tukaangukia kisiwani. Pana ndege wengi. Tukatafuta matunda tukala, tukatafuta na maji tukanywa. Hatta usiku, tukapanda juu ya mti tukalala. Alfajiri tukaingia mashuani mwetu, tukapotea, tukafika kisiwa kingine cha pili, hapana mtu awaye yote. Tukashuka, tukala matunda mengi, hatta usiku tukapanda juu ya mti, tukalala, wakaja nyama mbwayi, wakacheza sana.

Hatta assubui tukakimbia, tukaenda kisiwa cha tatu, tukifika tukitafuta matunda, tukaona mtofaa umezaa sana. Tukitaka kuchuma, tukasikia mtu, akatukataza, akinena, msichume, mtofaa u wa mwenyewe mfalme, nimewekwa kuungojea. Hatta usiku, wakaja kima wengi, wakafurahi sana walipotuona sisi, wakatutafutia matunda wakaletea, tukaja, tukala, hatta tukashiba.

Wakasema, mtu huyu tumfanye Sultani wetu. Yule mmoja akanena, watakimbia assubui hawa. Wakasema, kaivunjeni mashua yao. Wakaenda, wakaivunja.

Hatta assubui tukiondoka kukimbia, tukaenenda pwani, mashua yetu imevunjwa. Bassi, tukarudi, tukakaa kitako wakatuletea chakula, tukala, na maji, tukanwa. Na wale kima wanatupenda sana sisi, hawatupendi kuondoka. Siku nyingi tukakaa.

Hatta siku moja tukaenda kutembea, tukaona nyumba