Page:Swahili tales.djvu/368

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
348
HASSIBU KARIM AD DINI.

Akamwambia, miye ni mtoto wa Sultani, baba yangu amekufa, nimetawala mimi. Hatta siku moja nikafungua kasha la baba, nikaona mkoba, ndani na chuo, nikasoma chuo kile, nikaona sifa za mtume, nikafanya shauko sana ya kumwona, nikatoka mimi katika mji wangu, nikapotea katika mwitu kumtafuta mtu huyo. Na kulla mtu nimwonaye huniambia, hajazaliwa bado. Na hatta sasa ni katika mtafuta bado. Nikali nikienda katika barra.

Akamwambia, kaa kitako bassi, nikupe kisa changu toka mwanzo hatta sasa. Akamwambia, nipe, nimekwisha kaa kitako.

Akamwambia, mimi, jina langu Jani Shah, na baba yangu, jina lake Taighamusi, Sultani mkubwa. Naye kulla siku ikipata mwezi huenda mwituni kwenda kupiga nyama. Na mwanawe ni mimi tu mmoja, anipenda sana. Hatta siku hiyo nikamwambia, baba, tufuatane mwituni. Akaniambia, kaa kitako, usiende mahali. Nikalia sana mimi, baba yangu akaniambia, twende, usilie.

Tukaenda zetu mwituni, na watu wengi wanaokwenda. Hatta tulipofika mwituni tukala chakula, tukaisha, bassi kulla mtu tukaingia mwituni tupige nyama.

Na mimi na watumwa wangu, watu sabaa, tukaenda njia yetu ngine, hatta tukifika mwituni, tukaona paa mzuri mno tukamfukuza hatta baharini, tusimpate. Akaingia majini paa, tukatwaa mashua, tukaingia mimi na watumwa wangu watu wanne, wale watatu wakarudi kwa baba. Sisi tukamfukuza paa hatta tusiuone mji, tukamkamata paa, tukamchinja. Tulipokwisha mchinja, ukavuma upepo mwingi, tukapotea.

Wale watumwa, wale watatu, walipofika kwa baba yangu, akawauliza, yu wapi bwana wenu? Wakamwambia,