Jump to content

Page:Swahili tales.djvu/362

From Wikisource
This page has been proofread.
342
HASSIBU KARIM AD DINI.

yangu Sultani amekufa, nikaenda kufungua kasha, nikaona mkoba, nikaufungua, umetiwa kisanduku cha shaba, nikafungua, ndani umefungwa kwa joho, nikafunua joho, nikaona chuo, nikasoma mimi, nikaona sifa nyingi za mtume. Nikafanya shauko kumwona mtu huyu. Nikawauliza watu, wakaniambia, bado hajazaliwa. Nikasema, mimi nitapotea hatta nimwone. Nikaacha mji wangu na mali yangu, ni katika kupotea hatta sasa sijamwona mtu huyo.

Na mimi nikamwambia, utamwona wapi, hajazaliwa bado? Labuda ungalipata maji ya nyoka, ungaliweza kuishi, usife, hatta ukaonana naye, lakini sasa haifai, yako mbali maji ya nyoka.

Akaniambia, kua heri tena, nitapotea mimi. Nikamwambia, kua heri. Akaenda zake.

Hatta akafika Misri, akamwona mtu, akamwuliza, weye nani? Akamwambia, mimi Bolukia. Akamwuliza, na weye nani? Akamwambia, mimi jina langu Alfán. Akamwambia, unakwenda wapi? Akamwambia, mimi nimeacha mji wangu, na ufalme wangu, na mali yangu, namtafuta mtume.

Akamwambia, utamwona wapi weye, naye hajazaliwa bado? Lakini sasa tukamtafute Sultani wa nyoka, tukimpata huyu, atatupa dawa sisi tutakwenda hatta alipo nebii Sulimani; tutapata pete yake, tutawale sisi, na Majini yote yatakuwa chini yetu, tutakalo tutawaamru.

Akamwambia, mimi nimemwona Sultani wa nyoka katika jabali Al Káf. Akamwambia, twenende bass. Na yule Alfán moyoni mwake anataka pete ya nabii Sulimani apate kutawala, yee awe mfalme wa Majini na ndege. Yule Bolukia ataka kumwona mtume, ndio shauko yake.