Page:Swahili tales.djvu/358

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
338
HASSIBU KARIM AD DINI.

siku, yule humpelekea mchele, yule humpelekea mafuta, humpelekea kitoweo, humpelekea nguo, kulla siku.

Bassi hapa, turejee aliko Hassibu.

Amekaa siku ya kwanza, siku ya pili, siku ya tatu, akajua wenziwe wamemtupa, akashukuru Muungu. Akatembea ndani ya shimo, shimo kubwa sana. Usiku hulala mlemle, assubui akiamka, hupata asali kidogo, akala. Hatta siku moja amekaa kitako anawaza, akaona nge akaanguka chini, mkubwa sana, akamwua.

Akakaa kitako, akafikiri, nge huyu anatoka wapi? Labuda pana tundu mahala, nitakwenda kutafuta. Akaenda, akaona tundu ndogo, aona mwangaza mbali sana, akachokora kwa kisu, ikawa tundu pana sana, akapita, anaona mbali weupe na mwangaza, akaenda. Hatta akifika, akaona kiwanja, ametokea mahala pakubwa sana.

Akaona njia, akafuata njia, akaenda, akaona nyumba kubwa ya mawe, akaona na viti vingi, na mlango wake wa thahabu, na kufuli yake ya thahabu, na ufunguo wake wa lulu, akatwaa, akafungua, ndani akaona sébule kubwa, na viti vingi, akaona kiti kimoja cha thahabu, kimenakishiwa kwa lulu na jawahir na fusfús, akaona na kitanda kimetandikwa sana vizuri, akaenda akalala.

Hatta marra hiyo asikia watu wanakuja wengi. Wakaja hatta nyumbani, wakaona mlango umefunguliwa, wakaingia ndani. Na yule anayekuja ndiye Sultani wa nyoka.

Asikari wake wakajaa uwanjani, yee na mawaziri wake wakapita ndani, wakaona ajabu, wakamwona mtu amelala