Page:Swahili tales.djvu/352

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.

KISA CHA HASSIBU KARIM AD DINI NA SULTANI WA NYOKA.


Aliondokea mtu mganga sana, akakaa, hatta mwana mtoto asipate, siku nyingi. Naye tabibu mkuu, haina dawa moja ya ulimwenguni asiyoijua. Na elimu nyingi anayoijua. Akakaa, hatta alipokuwa mzee sana mkewe akachukua mimba, naye hana kitu zayidi ya vyuo vya dawa.

Akaugua yule mtu, akamwita mkewe, akamwambia, nipe chuo changu, akampa, akafunua akatezama ndani ya chuo, akamwambia, wewe una mimba, utazaa mtoto mwanamume, jina lake mwite Hassibu karim ad dini. Akafa babaye.

Akakaa manamke, hatta akazaa mtoto mwanamume, akamlea, hatta akawa mkubwa.

Yule mtoto akamwambia mamaye, jina langu nini? Akamwambia, ngoja, kesho tutafanya karamu, tutawaita watu, waje wale, nipate kukupa jina alionipa babayo.

Akakaa, assubui akafanya karamu kubwa, akawaita wanajimu, wakaja kula karamu, akawaambia, mtoto wenu leo nitampa jina alionipa babaye. Wakamwambia, mpe.