Page:Swahili tales.djvu/348

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
328
KITITI, NA FISI, NA SIMBA.

wakamwuliza, Wawaza nini. Akasema, Nawaza vile watu wakivaa nguo mpya, zile nguo kukuu kuenenda wapi? Wale wenziwe wakanena, Ni kweli maneno haya.

Wakaenenda tena, walipofika mbele fisi naye akasita. Wale wenziwe wakanena, Fisi amesita, na aliwe. Yule fisi akasema, Je! kwamba nawaza. Wale wenziwe wakamwuliza, Wawaza nini? Akasema, Siwazi hatta kitu. Wale wenziwe wakamtwaa fisi wakamla.

Akasalia simba na kititi, wakaenenda tena. Walipofika mbele wakaona mahali pana paango. Yule kititi akasita. Simba akasema, Kititi amesita, na aliwe. Yule kititi akasema, Je! kwamba nawaza. Simba akamwuliza, Wawaza nini? Akanena, Nawaza ile paango, hapo zamani za kale, wazee wetu walikuwa wakiingia kwa huku wakitokea kwa huku, nami nitakwenenda jaribu niingie kwa huku, nitokee kwa huku. Akaenenda akiingia kwa huku, akitokea kwa huku marra nyingi.

Akamwambia simba, Mzee simba, nawe enende ukajaribu uingie kwa huku utokee kwa huku. Yule simba akaenenda akaingia katika paango, akasakama asiweze kuenenda mbele wala kurudi nyuma. Yule kititi akaenenda maungoni mwa simba akamla nyama. Alipokwisha mla, yule simba akamwambia, Ndugu, unile upando wa mbeleni. Yule kititi akanena, Siwezi kuja kukula upande wa mbeleni, mato yaona haya.

Yule kititi akaenda zake, akamwata simba papale, na shamba lao akatwaa yeye.