Page:Swahili tales.djvu/346

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.

KITITI, NA FISI, NA SIMBA.


Hapo kale aliondoka simba, na kititi, na fisi, wakafanya mashauri kuenenda mashamba kulima. Wakaenenda hatta mashamba, wakalima wakapanda vyakula, baadaye wakarejea katika maskani yao wakakaa.

Hatta ilipowadia wakati wa kuiva vyakula, wakanena, Na twendeni shamba, tukaangalie vyakula vyetu. Na hilo shamba lao lilikuwa mbali sana. Yule kititi akawaambia wenziwe, zamani tutakapokwenenda shamba tusisite katika ndia, atakayesita na aliwe. Wale wenziwe wakakubali maneno hayo.

Bassi wakaenenda hatta walipofika ndiani, yule kititi akasita. Wale wenziwe wakanena, Kititi amesita na aliwe. Yule kititi akasema, Je! kwamba nawaza. Wale wenziwe wakamwuliza, Wawaza nini? Akasema, Nawaza yale mawe mawili, moja kubwa na moja dogo, lile dogo halendi juu, wala lile kubwa halendi tini. Wale wenziwe wakanena, Ni kweli maneno haya.

Wakaenenda tena, walipofika mbele, kititi akasita tena. Wale wenziwe wakasema, Kititi amesita, na aliwe. Yule kititi akanena, Je! kwamba nawaza. Wale wenziwe