Page:Swahili tales.djvu/342

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
322
UZA GHALI.

waliniambia wewe, uza ghali si uza rakhisi, na khati ya waziri hii alioniandikia, nawe soma, Sultani, ujue mambo haya kweli.

Sultani akaishika akaisoma khati, akamwambia, kweli, Ali, umekuza ghali hukuza rakhisi.

Akaondoka Sultani akamwita waziri. Akamwambia, lebeka hababi. Akawaambia watu, mlioko katika baraza, mkubwa na mdogo, na Banyani, na Mwarabu, na Msheheri, na Mngazidja, na Mswahili, na jamii ya watu waliomo katika inchi—bassi mimi nimemwondoa, hamo katika uwaziri wala katika usultani, hali yake kaiua hali ya waliyo katika mji. Na sasa huyu Ali ndiye amekuwa waziri wangu mkubwa, killa mtu atakalo, akiwa mume, akiwa mke, akiwa Mwarabu, akiwa Mzungu, wote na waende kwa Ali ndio atakokwisha mambo yenu.

Na hii hadithi imetokana na Ninga.