Page:Swahili tales.djvu/340

From Wikisource
Jump to navigation Jump to search
This page has been proofread.
320
UZA GHALI.

Sultani. Ali akanena, Ee Walla, ni kama Sultani, Sultani wangu.

Akaondoka Ali akapanda darini, akamwita—Mrashi, nitezamie katika nguo njema ziliomo katika makasha, kwani wewe ndiye ujuaye zayidi kuliko mgine. Akaenda Mrashi akifungua kasha akitoa joho mzuri, akatoa kilemba kizuri, akatoa na deuli aali akatoa na janvia moja la temsi la thahabu, akatoa na kitara kimoja cha albunsayidi cha Arabu, akatoa na kitupa cha hal wáradi Stambuli, akampelekea bwana.

Alipoziona Ali nguo zile akafurahi, akatwaa, akavaa, akishuka na yule Mwarabu, wakaenenda hatta wakafika katika mwango wa Sultani. Wakamwambia, pita sebulani. Akapita, akakaa kitako.

Akishuka yule Sultani kuja chini kubarizi, akashuka na yule aliokuwa Sultani kwanza, sasa aliokuwa waziri. Akamwambia waziri, akaitika, na'am. Akamwuliza, zile sharti zetu hazikufaa, nalikwambia mimi sharti zangu ujue kwa akili yako usiende kumwuliza Ali? Akamwambia, naam. Na wewe ukazunguka, ukaenda kumwuliza Ali. Akamwambia Sultani, sikumwuliza Ali. Sultani akanena, Ah! Ali si huyu yuko? Akamwambia, tumwite, aje mbele zako tupate kusadiki kama maneno haya kuyajua kwa akili yako wewe, ila kwa Ali kukwambia. Akamwambia, na'am, mwita Ali aje.

Akaondoka Sultani, akamwita Ali. Akamwambia, lebeka, hababi. Akamwambia, njoo. Akamwambia, gissi gani wewe, Ali, kwenda kukaa katika nyumba ya waziri, una maana gani? Akamwambia, na'am, Sultani,